PDF Print E-mail

SIKU MAALUMU YA KUOMBA NA KUCHANGIA MSTV

 

Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania, limeitenga siku ya Sabato ya Terehe 01-11-2014 kuwa siku maalumu kwa ajili ya kuomba na kuchangia kituo cha Televisheni cha kanisa hilo nchini kinachomilikiwa na washiriki.

 

Kituo hiki kwa sasa kinarusha matangazo yake kwa majaribio katika kisimbusi cha Digitek na TING.

Televisheni hii inahitaji kiasi cha Tsh milioni 225 kwa ajili ya kulipia gharama za kuwa hewani na pia kununua vifaa vya kurusha matangazo ya moja kwa moja.

 

Kwa maelezo zaidi wasiliana nao kwa namba hii +255 769 07 07 14

 

MUNGU AKUBARIKI SANA UNAPOTAFAKARI KUCHANGIA KITUO HIKI